Duration 2:53:1

BAJETI KUU YA SERIKALI 2021/2022

13 612 watched
0
77
Published 10 Jun 2021

#Bajeti #Bunge #Mwigulu Bajeti Kuu ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mwaka wa fedha 2021/2022 imewasilishwa Juni 10, 2021 Bungeni katika Bunge la Tanzania jijini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba.​ BAJETI 2021/22 YAPENDEKEZA BAJAJI NA BODABODA ZITOZWE TSH. 10,000 KWA KILA KOSA - Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu amependekeza adhabu kwa makosa ya maderebva wa bodaboda na bajaji kushuka kutoka Tsh. 30,000 HADI Tsh. 10,000 - Amesema faini ya Tsh. 30,000 imekuwa ikiwashinda vijana wengi ambapo wengi huzitelekeza pikipiki zao kwenye vituo vya polisi BAJETI 2021/22 YAPENDEKEZA TOZO KWENYE LAINI ZA SIMU KULINGANA NA UWEZO WA KUWEKA SALIO - Waziri wa Fedha, Dkt. Mwigulu Nchemba, amependekeza kutoza tozo ya Tsh. 10 hadi Tsh. 10,000 katika kila muamala wa kutuma au kutoa pesa - Pia, kutoza kiasi cha Tsh. 10 hadi Tsh. 200 kwa siku kwa kila laini ya simu kulingana na uwezo wa kuongeza salio Waziri Mwigulu: Kujenga miundombinu ya Shule kwa kusubiri irushwe mitandaoni ndio tuone inatutia aibu Kusubiri Watoto wakose pa kwenda au wakose pa kukaa ndipo tukimbizane na kufukuzana ni ishara ya kutojipanga vizuri. Hili tusingependa liendelee kuwepo Waziri Mwigulu: Napendekeza kutoza ada ya Tsh. 40,000 kwenye kibali cha kupeleka Nyama nje ya Nchi bila kujali aina ya nyama badala ya ada ya Tsh. 100 kwa kilo moja ya Nyama ya Ng’ombe na Tsh. 50 kwa kilo moja ya Nyama ya Mbuzi na Kondoo Waziri Mwigulu: Napendekeza kufanya mabadiliko ya sheria ya michezo ya Kubahatisha kwa kupunguza kiwango cha kodi kwenye zawadi ya ushindi kutoka asilimia 20 hadi asilimia 15 ya ubashiri wa matokeo Lengo ni kuleta usawa wa utozaji kodi katika michezo hiyo BAJETI 2021/22 YAPENDEKEZA GHARAMA ZA USAJILI WA NAMBA BINAFSI ZA MAGARI KUPUNGUA Waziri amependekeza usajili kupungua kutoka Tsh. Milioni 10 hadi Tsh. Milioni 5 kila miaka 3 Asema kiwango cha Tsh. Milioni 10 hakikuwa na mwitikio mzuri BAJETI 2021/22 YAPENDEKEZA KODI ZA MAJENGO ZIKUSANYWE KUPITIA LUKU Waziri wa Fedha amependekeza hilo kwasababu kila mita ya Umeme ina uhusiano na Mmiliki wa jengo au mtumiaji wa mita Apendekeza kodi iwe Tsh. 1,000 kwa nyumba za kawaida na Tsh. 5,000 kwa ghorofa

Category

Show more

Comments - 6